/*

Friday, 23 September 2016

Njia Unazoweza kutumia kupata Mtaji wa Biashara.


Leo Tutazungumzia Njia unazoweza Kuzitumia katika kupata Mtaji Wa Kuanzisha biashara.Mtaji umekuwa ni Kisingizio kikubwa kinachowazuia watu kufanya Biashara.Nakiita kisingizio kwani sio kweli na Haiwezekani mtaji kuwa kikwazo cha biashara kwa Mtu aliyekusudia hasa kufanya biashara.
Kabla ya kutaja njia unazoweza kuzitumia ili kupata mtaji wa Biashara kwanza nataka ufahamu kuwa,Mtaji Mkubwa kabisa unaohitajika katika kuanzisha Biashara si fedha Bali ni

Wewe Mwenyewe kuwa tayari,Baada ya kufahamu Mtaji Mkubwa unaohitajika ili kuanza biashara,Sasa unaweza kutafuta ni njia gani Utumie Ili kupata Mtaji wa kifedha.Zifuatazo ni baadhi ya njia unazoweza Kutumia kupat Mtaji wa  kuanzia biashara.
1.Kuweka kidogokidogo.
Hii ndio njia namba moja inayofaa kutumia ili kuweza kupata mtaji wa Biashara.Bila kujali ni kiasi gani unaingiza kwa siku,ni lazime ujihakikishie kuwa sehemu chache ya kiasi hiko unakiweka.Weka kuanzia asilimia 10 hadi 25 ya kipato chako cha kila siku au kila wiki au kila mwezi.Kwa mfano kama wewe kipato chako kwa mwezi ni TZS 300,000/= ikiwa utaweka asilimia 10 kila mwezi ambayo ni sawa na TZS 30,000/= kwa mwaka tayari utakuwa na TZS 360,000/= kwa miaka mitatu utakuwa na TZS 1,080,000/=,Kama Utaweka asilimia 20 ya kipato chako(Kwa wastani wa Kipato kwa mwezi cha TZS 300,000/=) kwa mwaka utakuwa umejiwekea  TZS 720,000/= na Kwa miaka mitatu ni TZS 2,160,000/=.Angalia kipato chako na chagua kiasi gani cha kuweka ambacho hakitaathiri Mahitaji yako lakini pia ambacho kitakufikisha katika Kiwango cha Mtaji Unachokihitaji.
2.Kuomba Fedha kutoka kwa Ndugu,Jamaa na Rafiki.
Kama njia iliyotangulia ni Ngumu kwako kutokana na kipato unachoingiza ni kile tu kinachoweza kukidhi Mahitaji yako na  hivyo unakosa cha kuweka,basi tumia Njia hii.Ondoa Aibu na Uwoga Na Uanze kuomba kiasi kutoka kwa Ndugu na jamaa,Ni vizuri zaidi uwe tayari umeshaandaa mpango wa Biashara yako na Kuwa muwazi uwaeleze kuwa Nini Kusudio lako.Bila shaka kwa kupitia Njia hii Unaweza kupata kiasi Cha kuanzia Biashara ya kawaida inayohitaji Mtaji wa kati.
3.Chukua Mkopo.
Kuchukua mkopo kutoka taasisi mbalimbali ili kuweza kuanzisha Biashara ni moja ya njia unazowez a Kutumia ili kupata Mtaji wa kuazisha Biashara.Ila njia hii ina changamoto nyingi sana.Wapo wanaoitumia na Wakafanikiwa na Wapo ambao Wanafeli kupitia njia hii.Angalia uthubutu wako na fanya maamuzi juu ya hili.Vilevile kikwazo kingine katika kutumia njia hii ni kwamba Taasisi nyingi za kifedha Zinahitaji Dhamana ya Mkopo Unaochukua hii itakuletea Shida kama Hauna mali ya Kuweka Dhamana.
4.Uza ulichonacho ambacho haukitumii.
Kama una kitu chochote cha Thamani ambacho haukitumii ni vema ukakiuza ili kupata Mtaji Wa kuaziasha Biashara.Au unaweza ukauza chochote ambacho unaona kuwa hakina umuhimu mkubwa kwa wakati Huo.Kwa Mfano Unamiliki TV,DVD Player,Laptop,Smartphone n.k kwa nini Usiuze Tv na DVD player ili upate Mtaji wa Biashara Ambao baada ya Muda mfupi Itakuingizia Faida na  kupata vitu zaidi ya Hivyo.Wapo wanaoamini kwamba kuuza ulichonacho ni kuukaribisha Umasikini hilo si sahihi,kwani inategemea Unauza ili Ufanye nini?
5.Anzisha  Biashara bila ya mtaji wa fedha.
Najua wengi watashangaa nitaanzaje biashara bila ya Mtaji wa fedha.Fahamu kuwa unaweza kutumia Nguvu zako ili kuweza kupata Fedha ambayo itakusaidia kuanzisha biashara.Hii inahitaji Uthubutu na kujitoa kwa kweli.

Tumia njia hizo Kupata Mtaji Wa kuanzisha Biashara Kama Ungependa Kujiajiri kupitia Internet,NIKUPONGEZE, utakuwa umeamua kuingia katika soko lililopanuka na lenye Wateja zaidi litakaloweza kukuingizia kipato kisicho na kikomo.
     Karibu Upate Ushauri na maelekezo kwa Gharama za Tsh.30,000/= Tu!Utapewa Mwongozo sahihi!! Utakaokufikisha katika Mafanikio.
.